Nyama nyekundu hatarini kutoweka kwa kukosekana maeneo ya malisho

Posted by:administrator in Farming, News

Tafiti zinaonyesha kuwa katika kipindi cha miaka kumi na tano ijayo mahitaji ya nyama nyeupe yataongezeka maradufu katika soko la nyama kufuatia upungufu wa maeneo ya malisho ya mifugo yenye nyama nyekundu kama Ng’ombe.

Akizungumza mjini Morogoro, katibu mkuu wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi anayeshughulikia mifugo Dr Mary Mashingo amesema kutokana na changamoto hiyo,  watanzania wanapaswa kujianda na ufugaji wa mifugo wengine ikiwemo Kuku na Nguruwe ambao ufugaji wake ni wa muda mfupi na hauna gharama, huku mwenyekiti wa chama cha wafugaji wa Nguruwe nchini, TAPIFA, Emmanuel Faustine akibainisha wamejiandaa kutumia fursa hiyo kwa kuleta mbegu mpya ya Nguruwe kutoka Afrika ya Kusini na Zambia zinazozaa kwa wingi.

Mwenyekiti wa bodi ya nyama Tanzania Prof, Faustin Lekule amesema kuwa aina ya mbegu za Nguruwe zilizochaguliwa kuingia nchini toka nje ni bora na magonjwa hupimwa kabla ya kuingizwa nchini kwa ajili ya matumizi, huku kaimu mkurugenzi wa uzalishaji wa mifugo na masoko toka wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi aron mziga akibainisha serikali kufanyia kazi sera ya mifugo ili kuendana na mazingira ya sasa.