Homa ya nguruwe (ASF) na jinsi ya kujikinga nayo

Posted by:humphrey

Ndugu Mfugaji Nini cha kufanya kukiwa na mlipuko wa homa ya Nguruwe(ASF)*

Kuna mambo ya kuzingatia ili ugonjwa usiingie shambani au usisambae

1.Kwa shamba ambalo lipo salama, zingatia sana *bio-security* ikiwa ni

✅Kuzuia matembezi shambani kwa watu na vyombo vya usafiri
✅Kupiga mabanda dawa zinazodhibiti vizuri na kutumia hizo kujisafisha mtu anapoingia mabandani au anaerudi toka nje ya shamba
✅Kudhibiti nzi na kunguru
✅kuepuka kununua vyakula na madawa sehemu sehemu wanauza rejareja.Hukonwatu wengi hufika na kipindi hiki ni hatari
✅Kuna unao mbwa/paka, wafunge wasitembee hovyo.Wasije kula mizoga na kurudi na ugonjwa
✅Epuka kutembelewa na madaktari wa mtaani,wapo busy sasa toka shamba moja kwenda jingine.Wengi hawajui kabisa habari ya bio-security
✅Usinunue wanyama wapya na kuleta shambani kwako kwa sasa.Hujui huko unakotoa kuna shida gani
✅Usiuze wanyama *wagonjwa*.Kama wana homa tayari utakuwa unasambaza ugonjwa

 

2.Kwa wale waliingiliwa na ugonjwa,hili jambo ni gumu sana na linaumiza!

✅Kama wanyama wanaumwa ASF usiuze.Ukiuza ama kwa mbegu au nyama unaendeleza kusambaza ugonjwa.Usambaze maumivu kwa watu wengine
✅Wanyama wanaoumwa wanatakiwa  kuchomwa moto au kufukiwa kwenye shimo refu
✅Kama ugonjwa uliingia kwako na kuna wanyama waliobaki,wanabaki na ugonjwa,wanakuwa carrier. Fanya utaratibu wa kuwatoa wanyama wote
✅Ukitaka kuanza tena mradi uwe na subira.Safisha mabanda kwa dawa zinazodhibiti Virus.Subiri angalia msimu mmoja wa kiangazi upite ndipo uanze kufuga tena.

NDUGU WAFUGAJI CHUKUENI TAHADHARI ILI MUWEZE KUJIKINGA NA HILI JANGA.!!!!!!